وَلَا تَقُولُواْ لِمَا تَصِفُ أَلۡسِنَتُكُمُ ٱلۡكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٞ وَهَٰذَا حَرَامٞ لِّتَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ لَا يُفۡلِحُونَ ١١٦
Walā taqūlū limā tasifu alsinatukumul-kadhiba hādhā halālun wahādhā harāmul litaftarū 'alallāhil-kadhiba innal-ladhīna yaftarūna 'alallāhil-kadhiba lā yuflihūn
Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali,na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa. 116
Maelezo ya chini
116 Na ilivyo kuwa Mwenyezi Mungu amekwisha kubainishieni kilicho halali na kilicho haramu, basi shikamaneni na hayo aliyo kubainishieni, wala msithubutu kuhalalisha na kuharimisha ovyo kufuata ndimi zenu. Mkawa mnasema: Hichi halali, na hichi haramu. Matokeo ya hizo kauli zenu ni kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na kumkhusisha na asiyo yasema! Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawapati kheri wala mafanikio.