وَلَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مِّنۡهُمۡ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُ وَهُمۡ ظَٰلِمُونَ ١١٣
Walaqad jā'ahum rasūlum minhum fakaddhabūhu fa akhadhahumul-'adhābu wahum zālimūn
Na alikwisha wajia Mjumbe wa miongoni mwao wenyewe. Lakini wakamkanusha;basi iliwafika adhabu hali ya kuwa wamedhulumu. 113
Maelezo ya chini
113 Nao alikwisha wajia Mtume kutokana nao wenyewe. Ilikuwa ni waajibu wao wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hayo, lakini walimwambia mwongo, kwa inda na husda tu. Adhabu ikawatwaa nao hali wamo katika udhalimu, na kwa sababu ya hiyo dhulma.