فَكُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلٗا طَيِّبٗا وَٱشۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ إِيَّاهُ تَعۡبُدُونَ ١١٤
Fakulū mimmā razaqakumullāhu halālan tayyiban washkurū ni'matallāhi in kuntum iyyāhu ta'budūn
Basi kuleni katika vile alivyo kupeni Mwenyezi Mungu, vilivyo halali na vizuri. Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye. 114
Maelezo ya chini
114 Ikiwa washirikina wanazikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wanazigeuza kuwa ni nakama, basi nyinyi Waumini elekeeni kwenye shukra. Na kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu na akakufanyieni kuwa ni vizuri kwenu, wala msijiharimishie nafsi zenu. Na ishukuruni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu kwa kumt'ii Yeye tu peke yake, ikiwa kweli mnamkusudia Yeye tu kwa ibada.