Surat An-Nahl, aya 106

16:106

مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ إِيمَٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنۡ أُكۡرِهَ وَقَلۡبُهُۥ مُطۡمَئِنُّۢ بِٱلۡإِيمَٰنِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلۡكُفۡرِ صَدۡرٗا فَعَلَيۡهِمۡ غَضَبٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٞ ١٠٦

Man kafara billāhi mim ba'di īmānihī illā man ukriha waqalbuhū mutma'innu bil-īmāni walākim man sharaha bil-kufri sadran fa'alayhim ghadabum minallāhi walahum 'adhābun 'azīm

Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipo kuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa. 106

Maelezo ya chini

106 Hao wanao tamka ukafiri baada ya kuamini watapata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Isipo kuwa aliye lazimishwa kutamka maneno ya ukafiri na hali moyo wake umesimama imara katika Imani. Huyo atavuka, haitompata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Ama ambao nyoyo zao zinafurahia ukafiri, na ndimi zao zinakubaliana na yaliyo nyoyoni mwao, hao watapata ghadhabu kali kwa Mwenyezi Mungu ambaye amewaandalia adhabu kubwa katika Akhera.