وَقِيلَ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ فَدَعَوۡهُمۡ فَلَمۡ يَسۡتَجِيبُواْ لَهُمۡ وَرَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۚ لَوۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ يَهۡتَدُونَ ٦٤
Waqīlad'ū shurakā'akum fada'awhum falam yastajībū lahum wara'awul-'adhāba law annahum kānū yahtadūn
Na itasemwa: Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu! Basi watawaita, lakini hawatawaitikia, na wataiona adhabu; laiti wangeli kuwa wameongoka! 64
Maelezo ya chini
64 Na Mwenyezi Mungu kuwaamrisha makafiri ni kwa kuwatahayarisha tu, kwa vile kuwataka wawaite wale miungu ya ushirikina wawaokoe na adhabu yake, kama walivyo dai. Wakaitikia kwa unyonge, na wakawaita kwa kuwa hawana hila. Wasipate jawabu yoyote. Wakaiona adhabu walio ahidiwa iko mbele yao, na wakatamani lau kuwa katika dunia yao wangeli kuwa Waumini walio ongoka, jinsi ya adhabu iliyo wafikia.