قَالَ ٱلَّذِينَ حَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقَوۡلُ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَغۡوَيۡنَآ أَغۡوَيۡنَٰهُمۡ كَمَا غَوَيۡنَاۖ تَبَرَّأۡنَآ إِلَيۡكَۖ مَا كَانُوٓاْ إِيَّانَا يَعۡبُدُونَ ٦٣
Qālal-ladhīna haqqa 'alayhimul-qawlu rabbanā hā'ulā'il-ladhīna aghwaynā aghwaynāhum kamā ghawaynā tabarra'nā ilayka mā kānū iyyānā ya'budūn
Watasema wale iliyo thibiti juu yao kauli: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio tulio wapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyo potea sisi. Tunajitenga nao mbele yako. Hawakuwa wakituabudu sisi. 63
Maelezo ya chini
63 Watasema waongozi wa makafiri katika walio stahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na vitisho vyake: Ewe Mola wetu Mlezi! Hawa tulio waita kwenye shirki na tukawapambia upotovu tuliwapoteza. Kwa sababu wao walikhiari ukafiri na wakaupokea, kama sisi tulivyo ukhiari na tukaupokea. Leo sisi tunajitenga nao kwako na ukafiri walio ukhiari duniani. Hawakuwa wao wakituabudu sisi; bali wakiabudu pumbao zao, na wakit'ii matamanio yao.