إِنَّكَ لَا تَهۡدِي مَنۡ أَحۡبَبۡتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِٱلۡمُهۡتَدِينَ ٥٦
Innaka lā tahdī man ahbabta walākinnallāha yahdī man yashā'u wahuwa a'lamu bil-muhtadīn
Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao. 56
Maelezo ya chini
56 Ewe Mtume! Hakika wewe una pupa sana kutaka hawa watu wako waongoke. Lakini wewe huwezi kumuingiza katika Uislamu kila umpendaye. Lakini Mwenyezi Mungu humwongoa kuendea Imani yule anaye mjua kuwa ameelekea uwongofu na ameukhiari. Na Yeye ndiye Mwenye kujua, wala hapana ajuaye zaidi kuliko Yeye, nani atakaye ingia katika safu za wenye kuongoka.