Surat Al-Qasas, aya 23

28:23

وَلَمَّا وَرَدَ مَآءَ مَدۡيَنَ وَجَدَ عَلَيۡهِ أُمَّةٗ مِّنَ ٱلنَّاسِ يَسۡقُونَ وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ ٱمۡرَأَتَيۡنِ تَذُودَانِۖ قَالَ مَا خَطۡبُكُمَاۖ قَالَتَا لَا نَسۡقِي حَتَّىٰ يُصۡدِرَ ٱلرِّعَآءُۖ وَأَبُونَا شَيۡخٞ كَبِيرٞ ٢٣

Walammā warada mā'a madyana wajada 'alayhi ummatam minan-nāsi yasqūna wawajada min dūnihimumra'atayni tadhūdāni qāla mā khatbukumā qālatā lā nasqī hattā yusdirar-ri'ā'u wa abūnā shaykhun kabīr

Na alipo yafikia maji ya Madyana alikuta umati wa watu wananywesha (wanyama wao), na akakuta karibu yao wanawake wawili wanawazuia wanyama wao. Akasema: Mna nini? Wakasema: Hatunyweshi sisi mpaka wamalize hao wachunga. Na baba yetu ni mzee sana. 23

Maelezo ya chini

23 Alipo yafikia maji ya Madyana wanapo nyweshea maji alikuta karibu na kisima kundi la watu wengi mbali mbali wanawanywesha wanyama wao wa mifugo. Na pahali pa chini kuliko hapo pao akawakuta wanawake wawili wanawazuia kunywa maji kondoo na mbuzi wao. Musa akawaambia: Mbona mko mbali na maji? Wakajibu: Hatuwezi kusukumana, na wala hatunyweshi sisi mpaka hawa wachunga wamalize wao kunywesha. Na baba yetu ni mkongwe, hawezi kuchunga wala kunywesha wanyama.