رَّبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذۡهُ وَكِيلٗا ٩
Rrabbul-mashriqi wal-maghribi lā ilāha illā huwa fattakhidhhu wakīlā
Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipo kuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako. 9
Maelezo ya chini
9 Yeye ndiye Mwenye kumiliki mashariki na magharibi, hapana wa kuabudiwa kwa haki isipo kuwa Yeye. Basi mfanye Yeye tu ndiye wa kukutosha katika mambo yako yote, ndiye wa kutegemewa peke yake kama alivyo ahidi.