وَلَقَدۡ أَخَذۡنَٰهُم بِٱلۡعَذَابِ فَمَا ٱسۡتَكَانُواْ لِرَبِّهِمۡ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ ٧٦
Walaqad akhadhnāhum bil-'adhābi famastakānū lirabbihim wamā yatadarra'ūn
Na hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea. 76
Maelezo ya chini
76 Na Sisi kwa hakika tuliwapa adhabu kama kwa kuwauwa au kuwaletea njaa. Na wala hawakumnyenyekea Mola wao Mlezi, bali waliendelea na jeuri zao na kiburi chao kiasi ya kuondoka tu hiyo adhabu.