Surat Al-Ma'idah, aya 9

5:9

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٌ عَظِيمٞ ٩

Wa'adallāhul-ladhīna āmanū wa'amilus-sālihāti lahum maghfiratun wa ajrun 'azīm

Mwenyezi Mungu amewaahidi walio muamini na wakatenda mema kwamba watapata maghfira na malipo makubwa. 9

Maelezo ya chini

9 Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake amewaahidi walio isadiki Dini yake na wakatenda mema kuwa atawasamehe dhambi zao, na atawalipa badala yake thawabu.