Surat Al-Ma'idah, aya 54

5:54

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَن يَرۡتَدَّ مِنكُمۡ عَن دِينِهِۦ فَسَوۡفَ يَأۡتِي ٱللَّهُ بِقَوۡمٖ يُحِبُّهُمۡ وَيُحِبُّونَهُۥٓ أَذِلَّةٍ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ يُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوۡمَةَ لَآئِمٖۚ ذَٰلِكَ فَضۡلُ ٱللَّهِ يُؤۡتِيهِ مَن يَشَآءُۚ وَٱللَّهُ وَٰسِعٌ عَلِيمٌ ٥٤

Yā'ayyuhal-ladhīna āmanū man yartadda minkum 'an dīnihī fasawfa ya'tillāhu biqawmin yuhibbuhum wayuhibbūnahū adhillatin 'alal-mu'minīna a'izzatin 'alal-kāfirīna yujāhidūna fī sabīlillāhi walā yakhāfūna lawmata lā'imin dhālika fadlullāhi yu'tīhi man yashā'u wallāhu wāsi'un 'alīm

Enyi mlio amini! Atakaye iacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anao wapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa Waumini na wenye nguvu juu ya makafiri, wanapigania Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anaye laumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua. 54

Maelezo ya chini

54 Enyi mlio amini! Mwenye kurejea ukafirini katika nyinyi, baada ya kuamini, hamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. Yeye ametukuka na hayo. Badala yao ataleta kaumu iliyo bora kuliko hao, na wao hao Mwenyezi Mungu atawapenda, na atawafikisha kwenye uwongofu, na ut'iifu. Na wao watampenda Mwenyezi Mungu, kwa hivyo watamt'ii. Nao watakuwa na unyenyekevu na huruma kwa ndugu zao Waumini, na watakuwa wakali na wenye nguvu mbele ya maadui zao makafiri. Watapigana jihadi kwa njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama yoyote ya mwenye kulaumu! Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye anaye muwafikia kheri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa fadhila kwa anaye stahiki.