وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ جَعَلَ فِيكُمۡ أَنۢبِيَآءَ وَجَعَلَكُم مُّلُوكٗا وَءَاتَىٰكُم مَّا لَمۡ يُؤۡتِ أَحَدٗا مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ ٢٠
Wa idh qāla mūsā liqawmihī yāqawmidhkurū ni'matallāhi 'alaykum idh ja'ala fīkum ambiyā'a waja'alakum mulūkan wa ātākum mā lam yu'ti ahadam minal-'ālamīn
Na pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu, alipo wateuwa Manabii kati yenu, na akakufanyeni watawala, na akakupeni ambayo hakuwapa wowote katika walimwengu. 20
Maelezo ya chini
20 Na taja, ewe Mtume! pale Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu kwa kushukuru na kut'ii, kwa kuwa amewateua Manabii wengi miongoni mwenu, na akakufanyeni watukufu kama wafalme baada ya kuwa mlikuwa wanyonge chini ya utawala wa Firauni, na akakupeni neema nyingi nyenginezo ambazo hawajapewa wowote wengineo.