يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ قَدۡ جَآءَكُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ عَلَىٰ فَتۡرَةٖ مِّنَ ٱلرُّسُلِ أَن تَقُولُواْ مَا جَآءَنَا مِنۢ بَشِيرٖ وَلَا نَذِيرٖۖ فَقَدۡ جَآءَكُم بَشِيرٞ وَنَذِيرٞۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ ١٩
Yā'ahlal-kitābi qad jā'akum rasūlunā yubayyinu lakum 'alā fatratim minar-rusuli an taqūlū mā jā'anā mim bashīrin walā nadhīrin faqad jā'akum bashīrun wanadhīrun wallāhu 'alā kulli shay'in qadīr
Enyi Watu wa Kitabu! Bila ya shaka amekujilieni Mtume wetu akikubainishieni katika wakati usio kuwa na Mitume, msije mkasema: Hakufika kwetu mbashiri wala mwonyaji. Basi amekujieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu anao uweza wa kila kitu. 19
Maelezo ya chini
19 Enyi Watu wa Kitabu! Umekujieni ujumbe wa Mtume wetu ambaye anakudhihirishieni Haki, baada ya kusita ujumbe kwa muda wa zama, ili msitafute udhuru wa ukafiri wenu, kwa kudai ati kuwa Mwenyezi Mungu hakukuleteeni mbashiri wa kukupeni khabari njema, wala mwonyaji wa kukuhadharisheni. Sasa, basi, huyo amekujilieni mbashiri na mwonyaji. Na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila jambo - na katika hayo mambo ni kutuma Mitume, na kukuhisabuni kwa mliyo nayo.