مَا قُلۡتُ لَهُمۡ إِلَّا مَآ أَمَرۡتَنِي بِهِۦٓ أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ رَبِّي وَرَبَّكُمۡۚ وَكُنتُ عَلَيۡهِمۡ شَهِيدٗا مَّا دُمۡتُ فِيهِمۡۖ فَلَمَّا تَوَفَّيۡتَنِي كُنتَ أَنتَ ٱلرَّقِيبَ عَلَيۡهِمۡۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ ١١٧
Mā qultu lahum illā mā amartanī bihī ani'budullāha rabbī warabbakum wakuntu 'alayhim shahīdam mā dumtu fīhim falammā tawaffaytanī kunta antar-raqība 'alayhim wa anta 'alā kulli shay'in shahīd
Sikuwaambia lolote ila uliyo niamrisha, nayo ni: Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Na mimi nilikuwa shahidi juu yao nilipo kuwa nao. Na ulipo nifisha ukawa Wewe ndiye Muangalizi juu yao. Na Wewe ni shahidi juu ya kila kitu. 117
Maelezo ya chini
117 Mimi sikuwaambia ila uliyo niamrisha niwafikishie. Nimewaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake. Kwani Yeye ndiye Mwenye kumiliki mambo yangu na yenu. Na mimi nilikuwa naijua hali yao nilipo kuwa nao. Na ulipo malizika muda uliyo nikadiria nikae nao ulikuwa Wewe peke yako ndiye unaye wajua. Na Wewe ni Mwenye kujua kila kitu.