فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَيَآ أَهۡلَ قَرۡيَةٍ ٱسۡتَطۡعَمَآ أَهۡلَهَا فَأَبَوۡاْ أَن يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيهَا جِدَارٗا يُرِيدُ أَن يَنقَضَّ فَأَقَامَهُۥۖ قَالَ لَوۡ شِئۡتَ لَتَّخَذۡتَ عَلَيۡهِ أَجۡرٗا ٧٧
Fantalaqā hattā idhā atayā ahla qaryatinistat'amā ahlahā fa abaw an yudayyifūhumā fawajadā fīhā jidāran yurīdu an yanqadda fa aqāmahū qāla law shi'ta lattakhadhta 'alayhi ajrā
Basi wakatoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula, nao wakakataa kuwakaribisha. Hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka, (yule mja mwema) akausimamisha. (Musa) akasema: Ungeli taka ungeli chukua ujira kwa haya. 77
Maelezo ya chini
77 Wakenda hata wakafika kwenye mji. Wakawataka watu wake wawape chakula, wakakataa kuwakirimu. Wakakuta ukuta umeinama wakaribia kuanguka. Yule mja mwema akaudiriki. Akaujenga mpaka akausimamisha sawa. Musa akasema: Ungeli taka ungeli weza kudai ujira kwa kazi uliyo ifanya.