Surat Al-Kahf, aya 45

18:45

وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا كَمَآءٍ أَنزَلۡنَٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخۡتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلۡأَرۡضِ فَأَصۡبَحَ هَشِيمٗا تَذۡرُوهُ ٱلرِّيَٰحُۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ مُّقۡتَدِرًا ٤٥

Wadrib lahum mathalal-hayawātid-dunyā kamā'in anzalnāhu minas-samā'i fakhtalata bihī nabātul-ardi fa asbaha hashīman tadhrūhur-riyāhu wakānallāhu 'alā kulli shay'im muqtadirā

Na wapigie mfano wa maisha ya dunia. Hayo ni kama maji tunayo yateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi, kisha hiyo mimea ikawa vibuwa vinavyo peperushwa na upepo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. 45

Maelezo ya chini

45 Ewe Mtume! Watajie watu mfano wa maisha ya duniani, vipi uzuri wake na kupendeza kwake, na mara hupotelea mbali. Ni kama mfano wa maji yanayo teremka kutoka mbinguni yakamwagiwa mimea ikanawiri, ikastawi. Kisha punde si punde ikakauka, ikawa vibua vikavu vilivyo katika katika vikipeperushwa na upepo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuleta na kuondoa akitakacho.