Surat Al-Kahf, aya 46

18:46

ٱلۡمَالُ وَٱلۡبَنُونَ زِينَةُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَٱلۡبَٰقِيَٰتُ ٱلصَّٰلِحَٰتُ خَيۡرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابٗا وَخَيۡرٌ أَمَلٗا ٤٦

Al-mālu wal-banūna zīnatul-hayawātid-dunyā wal-bāqiyātus-sālihātu khayrun 'inda rabbika thawāban wakhayrun amalā

Mali na wana ni pambo la maisha ya dunia. Na mema yanayo bakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini. 46

Maelezo ya chini

46 Mali na wana ni pambo na starehe kwenu katika uhai wa duniani, na pia ndio nguvu zenu. Lakini vyote hivyo havina dawamu. Hivyo vina mwisho wake, havibakii. Na vitendo vyema vyenye kubaki ni bora kwenu mbele ya Mwenyezi Mungu. Yeye hukumimieni kwa ukarimu thawabu zake, na hivyo ndio bora ya matumaini ya binaadamu.