Surat Al-Kahf, aya 44

18:44

هُنَالِكَ ٱلۡوَلَٰيَةُ لِلَّهِ ٱلۡحَقِّۚ هُوَ خَيۡرٞ ثَوَابٗا وَخَيۡرٌ عُقۡبٗا ٤٤

Hunālikal-walāyatu lillāhil-haqqi huwa khayrun thawāban wakhayrun 'uqbā

Huko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora wa malipo, na mbora wa matokeo. 44

Maelezo ya chini

44 Kwani katika kila hali nusura iko kwa Mwenyezi Mungu wa Haki peke yake. Na Yeye Subhanahu ni Mwema kwa mja wake Muumini, humkirimu kwa malipo, na humfanyia mema matokeo yake.