Surat Al-Kahf, aya 42

18:42

وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِۦ فَأَصۡبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيۡهِ عَلَىٰ مَآ أَنفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُشۡرِكۡ بِرَبِّيٓ أَحَدٗا ٤٢

Wa uhīta bithamarihī fa asbaha yuqallibu kaffayhi 'alā mā anfaqa fīhā wahiya khāwiyatun 'alā 'urūshihā wayaqūlu yālaytanī lam ushrik birabbī ahadā

Yakateketezwa matunda yake, akabaki akipindua pindua viganja vyake, kwa vile alivyo yagharimia, na miti imebwagika juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingeli mshiriki Mola wangu Mlezi na yeyote! 42

Maelezo ya chini

42 Mwenyezi Mungu kampatiliza yule kafiri, akayateketeza mavuno yote ya kitalu chake, na hicho kitalu chenyewe akakiangamiza, na akang'oa hata mizizi yake. Yule kafiri akabakia akipindua pindua viganja vyake kwa kusikitikia gharama alizo zitoa katika kukiamirisha kitalu chake, na baadae kuja kikapatilizwa na uharibifu. Akatamani lau kuwa hakumshirikisha Mola wake Mlezi na yeyote.