Surat Al-Jathiyah, aya 16

45:16

وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَ وَرَزَقۡنَٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَفَضَّلۡنَٰهُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦

Walaqad ātaynā banī isrā'īlal-kitāba wal-hukma wan-nubuwwata warazaqnāhum minat-tayyibāti wafaddalnāhum 'alal-'ālamīn

Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote. 16

Maelezo ya chini

16 Ninaapa kwa hakika tumewapa Wana wa Israili Taurati, na hukumu iliomo ndani yake, na Unabii ulio funuliwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na tumewaruzuku kheri namna mbali mbali, na tumewafadhilisha wao katika neema nyingi juu ya viumbe vyote.