Surat Al-Isra, aya 78

17:78

أَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِدُلُوكِ ٱلشَّمۡسِ إِلَىٰ غَسَقِ ٱلَّيۡلِ وَقُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِۖ إِنَّ قُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِ كَانَ مَشۡهُودٗا ٧٨

Aqimis-salawāta lidulūkish-shamsi ilā ghasaqil-layli waqur'ānal-fajri inna qur'ānal-fajri kāna mashhūdā

Shika Swala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima. 78

Maelezo ya chini

78 Shika Swala zilizo faridhiwa, tangu kupinduka jua kati ya mbingu kuelekea upande wa machwea jua, mpaka kiza cha usiku. Na hizi ndizo Swala za Adhuhuri, Alasiri, Magharibi na Isha. Na pia shika Swala ya Alfajiri ambayo wanaishuhudia Malaika.