Surat Al-Isra, aya 61

17:61

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ قَالَ ءَأَسۡجُدُ لِمَنۡ خَلَقۡتَ طِينٗا ٦١

Wa idh qulnā lil-malā'ikatisjudū li'ādama fasajadū illā iblīsa qāla a'asjudu liman khalaqta tīnā

Na pale tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam. Wakamsujudia isipo kuwa Iblisi. Akasema: Je! Nimsujudie uliye muumba kwa udongo? 61

Maelezo ya chini

61 Na Mwenyezi Mungu anakumbusha asli ya kuumba na uadui baina ya mwanaadamu na Iblisi, pale alipo waambia Malaika: Msujudieni Adam kwa kumuamkia na kumhishimu kwa kumuinamia. Hapo hapo wakasujudu. Isipo kuwa Iblisi akakataa, na akasema kwa chuki: Vipi nimsujudie uliye muumba kwa udongo, na hali mimi umeniumba kwa moto. Mimi ni bora kuliko yeye.