Surat Al-Isra, aya 55

17:55

وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِمَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَلَقَدۡ فَضَّلۡنَا بَعۡضَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ عَلَىٰ بَعۡضٖۖ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا ٥٥

Warabbuka a'lamu biman fis-samāwāti wal-ardi walaqad faddalnā ba'dan-nabiyyina 'alā ba'din wa ātaynā dāwūda zabūrā

Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa Zaburi. 55

Maelezo ya chini

55 Na Mola wako Mlezi anajua vilivyo vyote viliomo mbinguni na ardhini, na anajua hali zao. Basi anawakhiari miongoni mwao kwa kuwapa Unabii awatakao. Naye amekukhiari wewe kwa kukupa Utume wake. Basi haiwafalii wao kuudhika na Unabii wako. Na hao Manabii si wote sawa sawa kwa daraja mbele yake Aliye tukuka shani yake. Bali baadhi yao ni bora kuliko wenginewe. Naye amewatukuza baadhi ya Manabii juu ya wengine kwa miujiza, na wingi wa wafwasi, si kwa ufalme. Basi alitukuzwa Daudi kwa kuwa kapewa Zaburi, si kwa kuwa kapewa ufalme. Basi hapana ajabu kuwa wewe, Muhammad, ukapata fadhila kubwa kabisa kwa kuwa umepewa Qur'ani.