Surat Al-Isra, aya 56

17:56

قُلِ ٱدۡعُواْ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُم مِّن دُونِهِۦ فَلَا يَمۡلِكُونَ كَشۡفَ ٱلضُّرِّ عَنكُمۡ وَلَا تَحۡوِيلًا ٥٦

Qulid'ul-ladhīna za'amtum min dūnihī falā yamlikūna kashfad-durri 'ankum walā tahwīlā

Sema: Waombeni hao mnao wadaia badala yake Yeye. Hawawezi kukuondoleeni madhara, wala kuyaweka pengine. 56

Maelezo ya chini

56 Waambie hawa wanao abudu viumbe na wanadai kuwa hao ni miungu badala ya Mwenyezi Mungu: Waombeni hao mnao waabudu inapo kuteremkieni shida, au mkakhofu kuwa itakushukieni. Hamtopata kwao chochote cha kukuondoleeni madhara yenu, wala kuyahamisha akapewa mwinginewe.