رَّبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِكُمۡۖ إِن يَشَأۡ يَرۡحَمۡكُمۡ أَوۡ إِن يَشَأۡ يُعَذِّبۡكُمۡۚ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ وَكِيلٗا ٥٤
Rrabbukum a'lamu bikum in yasha' yarhamkum aw in yasha' yu'addhibkum wamā arsalnāka 'alayhim wakīlā
Mola wenu Mlezi anakujueni vilivyo. Akipenda atakurehemuni, na akipenda atakuadhibuni. Na hatukukutuma ili uwe mlinzi juu yao. 54
Maelezo ya chini
54 Mola wenu Mlezi ndiye anaye jua vyema mwisho wa mambo yenu. Akipenda atakurehemuni kwa kukupeni tawfiki ya Imani, (uwezo wa kuamini) au akipenda atakupeni adhabu kwa kuikosa hiyo Imani. Wala Sisi hatukukupeleka wewe uwe ni mwakilishi wao kwa mambo yao, hata uwalazimishe kuamini. Bali tumekutuma uwe ni mbashiri kuwapa khabari njema wenye kusadiki, na mwonyaji kuwaonya wanao kanusha. Waachilie mbali, na waamrishe sahaba zako wawastahamilie.