Surat Al-Isra, aya 42

17:42

قُل لَّوۡ كَانَ مَعَهُۥٓ ءَالِهَةٞ كَمَا يَقُولُونَ إِذٗا لَّٱبۡتَغَوۡاْ إِلَىٰ ذِي ٱلۡعَرۡشِ سَبِيلٗا ٤٢

Qul law kāna ma'ahū ālihatun kamā yaqūlūna idhal labtaghaw ilā dhil-'arshi sabīlā

Sema: Lau kuwa wangeli kuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi wangeli tafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi. 42

Maelezo ya chini

42 Ewe Nabii! Ili kudhihirisha upotovu wa madai yao wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu, sema: Lau kuwa wapo miungu wengine pamoja na Mwenyezi Mungu kama wasemavyo, hao miungu wangeli tafuta njia kumfikilia huyo Mwenye Ufalme wa mwisho ili wapate kushindana naye.