وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ تِسۡعَ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۖ فَسۡـَٔلۡ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِذۡ جَآءَهُمۡ فَقَالَ لَهُۥ فِرۡعَوۡنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَٰمُوسَىٰ مَسۡحُورٗا ١٠١
Walaqad ātaynā mūsā tis'a āyāti bayyinātin fas'al banī isrā'īla idh jā'ahum faqāla lahū fir'awnu innī la azunnuka yāmūsā mashūrā
Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Waulize Wana wa Israili alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa!. 101
Maelezo ya chini
101 Na lau hawa watu wangeli letewa hizo ishara wazitakazo, wange zigeuzia uso, wala wasinge ziamini! Na Sisi tulimpa Musa Ishara tisa wazi. Na juu ya hivyo wakakufuru. Na Firauni akasema: Hakika mimi nakuona wewe, Musa, ni mtu uliye rogwa! Hizo ishara tisa ni: 1. Fimbo, 2. Mkono Mweupe, 3. Tufani, 4. Nzige na vyura na chawa na damu, 5. Ukame na upungufu wa mazao, 6. Kupasuka bahari, 7. Kutimbuka maji baharini, 8. Kuning'inia mlima kama kivuli, 9. Kusemezwa na Mola wake Mlezi.