قُل لَّوۡ أَنتُمۡ تَمۡلِكُونَ خَزَآئِنَ رَحۡمَةِ رَبِّيٓ إِذٗا لَّأَمۡسَكۡتُمۡ خَشۡيَةَ ٱلۡإِنفَاقِۚ وَكَانَ ٱلۡإِنسَٰنُ قَتُورٗا ١٠٠
Qul law antum tamlikūna khazā'ina rahmati rabbī idhal la amsaktum khashyatal-infāqi wakānal-insānu qatūrā
Sema: Lau kuwa nyinyi mnazimiliki khazina za rehema za Mola wangu Mlezi, basi hapana shaka mngeli zuia kuzitumia kwa ajili ya kukhofu. Na mwanaadamu tangu hapo tabia yake ni mchoyo!. 100
Maelezo ya chini
100 Waambie hawa washirikina: Lau kuwa mnazimiliki riziki za Mola wangu Mlezi, mngeli zifanyia ubakhili kwa kuogopa ufakiri. Kwani ni tabia ya watu kuwa na pupa na ubakhili. Na Mwenyezi Mungu, Mkwasi na Karimu, humpa anacho taka amtakaye, na huteremsha miujiza aitakayo Yeye, sio waitakayo watu. Na Yeye katika yote hayo ni Mwenye hikima na Mjuzi.