إِنَّ ٱلَّذِينَ يَشۡتَرُونَ بِعَهۡدِ ٱللَّهِ وَأَيۡمَٰنِهِمۡ ثَمَنٗا قَلِيلًا أُوْلَٰٓئِكَ لَا خَلَٰقَ لَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ ٱللَّهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيۡهِمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ ٧٧
Innal-ladhīna yashtarūna bi'ahdillāhi wa aymānihim thamanan qalīlan ulā'ika lā khalāqa lahum fil-ākhirati walā yukallimuhumullāhu walā yanzuru ilayhim yawmal-qiyāmati walā yuzakkīhim walahum 'adhābun alīm
Hakika wanao uza ahadi ya Mwenyezi Mungu na viapo vyao thamani ndogo, hao hawatakuwa na sehemu ya kheri yoyote katika Akhera, wala Mwenyezi Mungu hatasema nao wala hatawatazama Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, nao watapata adhabu chungu. 77
Maelezo ya chini
77 Wanao iacha ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo fungamana nao ya kuwa watazitimiza haki na watasimamia yaliyo waajibu, wala hawatoacha viapo vyao walivyo apa kuwa watatimiza - kwa thamani ndogo ya faida ya dunia, na ingawa kuu katika maoni yao, hao hawatakuwa na sehemu yoyote katika raha za Akhera. Mola wao Mlezi atawapuuza, wala hatowaangalia kwa jicho la rehema Siku ya Kiyama, wala hatowafutia dhambi zao, na watapata adhabu chungu ya kuendelea.