Surat Al-Imran, aya 180

3:180

وَلَا يَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦ هُوَ خَيۡرٗا لَّهُمۖ بَلۡ هُوَ شَرّٞ لَّهُمۡۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُواْ بِهِۦ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ وَلِلَّهِ مِيرَٰثُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ ١٨٠

Walā yahsabannal-ladhīna yabkhalūna bimā ātāhumullāhu min fadlihī huwa khayral lahum bal huwa sharrul lahum sayutawwaqūna mā bakhilū bihī yawmal-qiyāmati walillāhi mīrāthus-samāwāti wal-ardi wallāhu bimā ta'malūna khabīr

Wala wasidhani wale ambao wanafanya ubakhili katika aliyo wapa Mwenyezi Mungu katika fadhila zake kuwa ni kheri yao. Bali hiyo ni shari kwao. Watafungwa kongwa za yale waliyo yafanyia ubakhili Siku ya Kiyama. Na urithi wa Mbingu na Ardhi ni wa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote myatendayo. 180

Maelezo ya chini

180 Wasidhani wanao fanya ubakhili kwa mali aliyo waneemesha Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake, na hawayatoi katika yaliyo waajibu na njia za kheri, kuwa ubakhili huo ni kheri yao. Bali hiyo ni shari yenye matokeo mabaya juu yao. Watalipwa malipo maovu kabisa Siku ya Kiyama, na adhabu itawaganda kama kongwa au mnyororo aliyo fungwa nayo mfungwa shingoni mwake. Kila kiumbe kinamnyenyekea Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la, naye ndiye Mmiliki wao, na Yeye Aliye takasika anajua kila mnacho kitenda, na atakulipeni kwacho.