لَّقَدۡ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوۡلَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ فَقِيرٞ وَنَحۡنُ أَغۡنِيَآءُۘ سَنَكۡتُبُ مَا قَالُواْ وَقَتۡلَهُمُ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖ وَنَقُولُ ذُوقُواْ عَذَابَ ٱلۡحَرِيقِ ١٨١
Llaqad sami'allāhu qawlal-ladhīna qālū innallāha faqīrun wanahnu aghniyā'u sanaktubu mā qālū waqatlahumul-ambiyā'a bighayri haqqin wanaqūlu dhūqū 'adhābal-harīq
Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya walio sema: Mwenyezi Mungu ni masikini, na sisi ni matajiri. Tumeyaandika waliyo yasema, na pia kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na tutawaambia Siku ya Kiyama: Onjeni adhabu ya kuungua. 181
Maelezo ya chini
181 Juu ya kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kumiliki kila kiliomo mbinguni na ardhini na Yeye ndiye mrithi wa vyote, wamesema baadhi ya Mayahudi kwa kejeli: Mwenyezi Mungu ni fakiri, ndiyo akatutaka tutoe, na sisi ni matajiri tukitoa au tusitoe. Mwenyezi Mungu amekwisha isikia kauli yao hiyo, na ameisajili dhidi yao, kama alivyo sajili kuwauwa kwao Manabii kwa dhulma na ukhalifu na uadui. Naye atawaambia Siku ya Kiyama: Onjeni adhabu ya Moto unao waka!