مَّا كَانَ ٱللَّهُ لِيَذَرَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ عَلَىٰ مَآ أَنتُمۡ عَلَيۡهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ ٱلۡخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِۗ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُطۡلِعَكُمۡ عَلَى ٱلۡغَيۡبِ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَجۡتَبِي مِن رُّسُلِهِۦ مَن يَشَآءُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۚ وَإِن تُؤۡمِنُواْ وَتَتَّقُواْ فَلَكُمۡ أَجۡرٌ عَظِيمٞ ١٧٩
Mmā kānallāhu liyadharal-mu'minīna 'alā mā antum 'alayhi hattā yamīzal-khabītha minat-tayyibi wamā kānallāhu liyutli'akum 'alal-ghaybi walākinnallāha yajtabī mir rusulihī man yashā'u fa'āminū billāhi warusulihī wa in tu'minū watattaqū falakum ajrun 'azīm
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue wabaya na wema. Wala haiwi kwa Mwenyezi Mungu kukujuulisheni mambo ya ghaibu. Lakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitume wake amtakaye. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume yake. Na mkiamini na mkamchamngu mtakuwa na ujira mkubwa. 179
Maelezo ya chini
179 Haiwi kuwa Mwenyezi Mungu akuacheni enyi jamaa Waumini katika hali mliyo nayo ya mchanganyiko wa Muumini na mnaafiki, mpaka awatenganishe baina yenu kwa misukosuko na taabu ili mumwone mnaafiki khabithi na Muumini mwema. Wala sio mwendo wa Mwenyezi Mungu kumjuulisha yeyote katika viumbe vyake khabari za ghaibu. Walakini Mwenyezi Mungu humteua katika Mitume yake ampendaye akamjuvya anacho kitaka katika mambo yake ya ghaibu. Na nyinyi mkiamini na mkamcha Mola wenu Mlezi kwa kujilazimisha kumt'ii atakutieni katika Pepo iwe ndio malipo. Na hayo ndio malipo yaliyo bora na makubwa kabisa.