Surat Al-Imran, aya 167

3:167

وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ نَافَقُواْۚ وَقِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ قَٰتِلُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ أَوِ ٱدۡفَعُواْۖ قَالُواْ لَوۡ نَعۡلَمُ قِتَالٗا لَّٱتَّبَعۡنَٰكُمۡۗ هُمۡ لِلۡكُفۡرِ يَوۡمَئِذٍ أَقۡرَبُ مِنۡهُمۡ لِلۡإِيمَٰنِۚ يَقُولُونَ بِأَفۡوَٰهِهِم مَّا لَيۡسَ فِي قُلُوبِهِمۡۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يَكۡتُمُونَ ١٦٧

Waliya'lamal-ladhīna nāfaqū waqīla lahum ta'ālaw qātilū fī sabīlillāhi awidfa'ū qālū law na'lamu qitālal lattaba'nākum hum lil-kufri yawma'idhin aqrabu minhum lil-īmāni yaqūlūna bi afwāhihim mā laysa fī qulūbihim wallāhu a'lamu bimā yaktumūn

Na ili awapambanue walio kuwa wanaafiki, wakaambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu au lindeni. Wakasema: Tungeli jua kuna kupigana bila ya shaka tungeli kufuateni. Wao siku ile walikuwa karibu na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao yasiyo kuwamo nyoyoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anajua kabisa wanayo yaficha. 167

Maelezo ya chini

167 Na hayo ili pia udhihiri unaafiki wa wanaafiki. Nao hawa ni wale walipo kuwa wanaondoka wanaacha vita wakaambiwa: Njooni mpigane kwa kumt'ii Mwenyezi Mungu, au kwa ajili ya kujilinda nafsi zenu. Wakasema: Lau kuwa tunajua kuwa mtakutana na vita, tungeli kwenda nanyi. Na wao walipo sema kauli hiyo walikuwa karibu zaidi na ukafiri kuliko Imani. Wanasema kwa midomo yao: Huko hakuna vita. Na hali wanaitakidi ndani ya nyoyo zao kuwa vita kweli vitakuwepo. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema unaafiki wanao uficha, kwani Yeye anajua matokeo ya siri zao.