وَلَقَدۡ صَدَقَكُمُ ٱللَّهُ وَعۡدَهُۥٓ إِذۡ تَحُسُّونَهُم بِإِذۡنِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَا فَشِلۡتُمۡ وَتَنَٰزَعۡتُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِ وَعَصَيۡتُم مِّنۢ بَعۡدِ مَآ أَرَىٰكُم مَّا تُحِبُّونَۚ مِنكُم مَّن يُرِيدُ ٱلدُّنۡيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ ٱلۡأٓخِرَةَۚ ثُمَّ صَرَفَكُمۡ عَنۡهُمۡ لِيَبۡتَلِيَكُمۡۖ وَلَقَدۡ عَفَا عَنكُمۡۗ وَٱللَّهُ ذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ١٥٢
Walaqad sadaqakumullāhu wa'dahū idh tahussūnahum bi idhnihī hattā idhā fashiltum watanāza'tum fil-amri wa'asaytum mim ba'di mā arākum mā tuhibbūna minkum man yurīdud-dunyā waminkum man yurīdul-ākhirata thumma sarafakum 'anhum liyabtaliyakum walaqad 'afā 'ankum wallāhu dhū fadlin 'alal-mu'minīn
Na Mwenyezi Mungu alikutimilizieni miadi yake, vile mlivyo kuwa mnawauwa kwa idhini yake, mpaka mlipo legea na mkazozana juu ya amri, na mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni mliyo yapenda. Wapo miongoni mwenu wanao taka dunia, na wapo miongoni mwenu wanao taka Akhera. Kisha akakutengeni nao (maadui) ili akujaribuni. Naye sasa amekwisha kusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya Waumini. 152
Maelezo ya chini
152 Nusura ya Mwenyezi Mungu ni jambo la hakika ya kweli. Mwenyezi Mungu ametimiza miadi yake kuwa alikupeni ushindi pale mara ya kwanza mlipo wauwa maadui wengi kwa radhi yake; mpaka yalipo dhoofika maoni yenu katika vita na mkakhitalifiana kuifahamu amri ya Nabii aliyo kupeni msiondoke kwenye vituo vyenu. Baadhi yenu mkaacha vituo vyenu mlipo ona mnashinda, na wengine wakabaki mpaka mwisho. Kikundi kimoja kikaasi amri ya Mtume kikenda kuwania ngawira baada ya kwisha kuonyeshwa mkipendacho, nao ni ushindi. Mkawa makundi mawili, wanao taka raha ya dunia, na wanao taka malipo ya Akhera. Ilivyo kuwa hivyo Mwenyezi Mungu akaondoa kwenu nusura yake, mkashindwa, ili akujaribuni, atambulikane mwenye ikhlasi na asiye kuwa nayo. Lakini sasa amekusameheni kwa kuwa mmejuta. Na Mwenyezi Mungu ana fadhila kwenu kwa kukusameheni na kukubali toba yenu.