۞ إِذۡ تُصۡعِدُونَ وَلَا تَلۡوُۥنَ عَلَىٰٓ أَحَدٖ وَٱلرَّسُولُ يَدۡعُوكُمۡ فِيٓ أُخۡرَىٰكُمۡ فَأَثَٰبَكُمۡ غَمَّۢا بِغَمّٖ لِّكَيۡلَا تَحۡزَنُواْ عَلَىٰ مَا فَاتَكُمۡ وَلَا مَآ أَصَٰبَكُمۡۗ وَٱللَّهُ خَبِيرُۢ بِمَا تَعۡمَلُونَ ١٥٣
Idh tus'idūna walā talwūna 'alā ahadin war-rasūlu yad'ūkum fī ukhrākum fa athābakum ghammā bighammil likaylā tahzanū 'alā mā fātakum walā mā asābakum wallāhu khabīru bimā ta'malūn
Pale mlipo kuwa mkikimbia mbio wala hamumsikilizi yeyote, na Mtume anakuiteni, yuko nyuma yenu. Mwenyezi Mungu akakupeni dhiki juu ya dhiki, ili msisikitike kwa yaliyo kukoseeni wala kwa yaliyo kusibuni. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda. 153
Maelezo ya chini
153 Enyi Waumini! Hebu ikumbukeni hali yenu wakati ule mlipo kuwa mkitoka mbio wala hamumsikii mtu kwa shida ya kukimbia; na Mtume anakuiteni nyuma yenu mrejee. Mwenyezi Mungu akakujazini huzuni ya kufudikiza kama wingu lilio funika nafsi zenu, ili msisikitike kwa ngawira mlizo zikosa wala kushindwa kuliko kusibuni. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema makusudio yenu na vitendo vyenu.