Surat Al-Imran, aya 151

3:151

سَنُلۡقِي فِي قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱلرُّعۡبَ بِمَآ أَشۡرَكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗاۖ وَمَأۡوَىٰهُمُ ٱلنَّارُۖ وَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلظَّٰلِمِينَ ١٥١

Sanulqī fī qulūbil-ladhīna kafarur-ru'ba bimā ashrakū billāhi mā lam yunazzil bihī sultānan wama'wāhumun-nāru wabi'sa mathwaz-zālimīn

Tutazitia khofu nyoyo za walio kufuru kwa vile walivyo mshirikisha Mwenyezi Mungu na washirika ambao hakuwateremshia hoja yoyote. Na makaazi yao ni Motoni; na maovu yaliyoje maskani ya wenye kudhulumu! 151

Maelezo ya chini

151 Yasikutieni unyonge yaliyo kupateni siku ya Uhud. Sisi tutaingiza khofu na vitisho katika nyoyo za maadui zenu kwa kuwa wao wamemshirikisha Mwenyezi Mungu na miungu mengine ambayo Mwenyezi Mungu hakuwateremshia hoja yoyote. Kwani Miungu hiyo hainufaishi wala haidhurishi kitu. Na makao yao yatakuwa Motoni Akhera, na maovu mno hayo makao ya madhaalimu.