Surat Al-Imran, aya 150

3:150

بَلِ ٱللَّهُ مَوۡلَىٰكُمۡۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلنَّٰصِرِينَ ١٥٠

Balillāhu mawlākum wahuwa khayrun-nāsirīn

Bali Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wenu, naye ndiye bora wa wasaidizi. 150

Maelezo ya chini

150 Mwenyezi Mungu ndiye wa kukunusuruni, basi msiwaogope hao binaadamu wenzenu, kwani Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa kunusuru.