Surat Al-Humazah, aya 1

104:1

وَيۡلٞ لِّكُلِّ هُمَزَةٖ لُّمَزَةٍ ١

Waylul likulli humazatil lumazah

Ole wake kila safihi, msengenyaji! 1

Maelezo ya chini

1 Atapata adhabu kali na maangamio huyo ambaye mtindo wake ni kuwafedhehi watu kwa kauli au kwa ishara, au kuwasengenya kuwavunjia hishima zao.