وَلَوۡلَآ أَن كَتَبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡجَلَآءَ لَعَذَّبَهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَاۖ وَلَهُمۡ فِي ٱلۡأٓخِرَةِ عَذَابُ ٱلنَّارِ ٣
Walawlā an kataballāhu 'alayhimul-jalā'a la'addhabahum fid-dunyā walahum fil-ākhirati 'adhābun-nār
Na lau kuwa Mwenyezi Mungu asingeli waandikia kutoka, angeli waadhibu katika dunia. Na katika Akhera watapata adhabu ya Moto. 3
Maelezo ya chini
3 Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hakuwahukumia kuwatoa majumbani kwao kwa sura hii ya kuchusha, basi hapana shaka angeli waadhibu katika dunia kwa shida zaidi kuliko huko kuwatoa. Na Akhera, wao watapata adhabu ya Moto, mbali huku kutolewa majumbani kwao duniani.