Surat Al-Hashr, aya 4

59:4

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ شَآقُّواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥۖ وَمَن يُشَآقِّ ٱللَّهَ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ٤

Dhālika bi annahum shāqqullāha warasūlahū waman yushāqqillāha fa innallāha shadīdul-'iqāb

Hayo ni kwa sababu walimpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumpinga Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. 4

Maelezo ya chini

4 Hayo yaliyo wapata duniani na yanayo wangojea Akhera ni kwa sabau ya kuwa wamemfanyia uadui Mwenyezi Mungu na Mtume wake, uadui mkubwa mno. Na mwenye kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu basi hawezi kupenya kuikimbia adhabu yake. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.