Surat Al-Hajj, aya 13

22:13

يَدۡعُواْ لَمَن ضَرُّهُۥٓ أَقۡرَبُ مِن نَّفۡعِهِۦۚ لَبِئۡسَ ٱلۡمَوۡلَىٰ وَلَبِئۡسَ ٱلۡعَشِيرُ ١٣

Yad'ū laman darruhū aqrabu min naf'ihī labi'sal-mawlā walabi'sal-'ashīr

Humuomba yule ambaye bila ya shaka dhara yake ipo karibu zaidi kuliko nafuu yake. Kwa hakika huyo ni mlinzi muovu, na rafiki muovu. 13

Maelezo ya chini

13 Badala ya Mwenyezi Mungu anamwomba ambaye madhara yake kwa kuharibu akili na kutawala mawazo ovyo ni karibu zaidi kwa nafsi kuliko kuitakidi msaada wake. Muabudiwa huyo ni muovu mno wa kumtaraji msaada, na muovu mno kumfanya rafiki.