Surat Al-Baqarah, aya 37

2:37

فَتَلَقَّىٰٓ ءَادَمُ مِن رَّبِّهِۦ كَلِمَٰتٖ فَتَابَ عَلَيۡهِۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ ٣٧

Fatalaqqā ādamu mir rabbihī kalimātin fatāba 'alayhi innahū huwat-tawwābur-rahīm

Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi wa kukubali toba na Mwenye kurehemu. 37

Maelezo ya chini

37 Adam na mkewe walitambua makosa yao na kujidhulumu nafsi zao. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfunza Adam baadhi ya maneno ya kutubia na kuomba msamaha na akayasema. Mwenyezi Mungu alimkubalia toba yake, na akamsamehe, kwani Yeye ni mwingi wa kukubali toba, naye ni Mwenye kuwarehemu waja wake wanyonge.