Surat Al-Baqarah, aya 236

2:236

لَّا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِن طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ مَا لَمۡ تَمَسُّوهُنَّ أَوۡ تَفۡرِضُواْ لَهُنَّ فَرِيضَةٗۚ وَمَتِّعُوهُنَّ عَلَى ٱلۡمُوسِعِ قَدَرُهُۥ وَعَلَى ٱلۡمُقۡتِرِ قَدَرُهُۥ مَتَٰعَۢا بِٱلۡمَعۡرُوفِۖ حَقًّا عَلَى ٱلۡمُحۡسِنِينَ ٢٣٦

Llā junāha 'alaykum in tallaqtumun-nisā'a mā lam tamassūhunna aw tafridū lahunna farīdatan wamatti'ūhunna 'alal-mūsi'i qadaruhū wa'alal-muqtiri qadaruhū matā'ā bil-ma'rūfi haqqan 'alal-muhsinīn

Hapana ubaya kwenu mkiwapa T'alaka wanawake ambao hamjawagusa au kuwabainishia mahari yao. Lakini wapeni cha kuwaliwaza, mwenye wasaa kadiri awezavyo na mwenye dhiki kadiri awezavyo - maliwaza kwa mujibu wa dasturi kuwa ni haki juu ya watendao mema. 236

Maelezo ya chini

236 Wala hapana dhambi kwenu enyi waume, wala hapana mahari juu yenu mkiwaacha wake kabla ya kuingia harusi na kabla hamjawatajia kiasi cha mahari. Lakini wapeni zawadi kama kuwapoza kuwapunguzia machungu ya moyo. Na hicho mnacho toa kiwe cha kuridhisha na kupendeza moyo. Tajiri atoe kwa kadiri ya wasaa wake, na fakiri kwa kadiri ya hali yake. Na zawadi hiyo ni katika a'mali za kheri wanazo jilazimisha nazo watu wenye muruwa na watu wa kheri na ihsani.