Surat Al-Baqarah, aya 19

2:19

أَوۡ كَصَيِّبٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فِيهِ ظُلُمَٰتٞ وَرَعۡدٞ وَبَرۡقٞ يَجۡعَلُونَ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِم مِّنَ ٱلصَّوَٰعِقِ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِۚ وَٱللَّهُ مُحِيطُۢ بِٱلۡكَٰفِرِينَ ١٩

Aw kasayyibim minas-samā'i fīhi zulumātun wara'dun wabarqun yaj'alūna asābi'ahum fī ādhānihim minas-sawā'iqi hadharal-mawti wallāhu muhītu bil-kāfirīn

Au ni kama mvua kubwa itokayo mbinguni, ina giza na radi na umeme; wakawa wakitia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili ya mingurumo, kwa kuogopa kufa. Na Mwenyezi Mungu amewazunguka makafiri. 19

Maelezo ya chini

19 Au mfano wa hali yao katika kubabaika kwao, na hadi ya mambo yanavyo waemea, na kutokufahamu nini liwafaalo na nini linalo wadhuru, ni kama hali ya watu walio teremkiwa na mvua kutoka mbinguni, yenye radi na mingurumo, wanatia ncha za vidole vyao masikioni mwao ili ati wasisikie sauti za mingurumo, na huku wanaogopa kufa, wakidhani kuwa kule kujiziba kwa vidole kutawalinda na mauti. Watu hao ikiteremka Qur'ani - na ndani yake ikabainisha giza la ukafiri na ikatoa maonyo ya juu yake, na ikabainisha Imani na mwangaza wake unao meremeta, na yakabainishwa mahadharisho na namna mbali mbali za adhabu - wao hujitenga nayo na wakajaribu kuepukana nayo kwa kudai kuwa ati kwa kujitenga nayo wataepukana na adhabu. Lakini Mwenyezi Mungu amewazunguka makafiri kila upande kwa ujuzi wake na uwezo wake.