فَمَنۡ خَافَ مِن مُّوصٖ جَنَفًا أَوۡ إِثۡمٗا فَأَصۡلَحَ بَيۡنَهُمۡ فَلَآ إِثۡمَ عَلَيۡهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ١٨٢
Faman khāfa mim mūsin janafan aw ithman fa aslaha baynahum falā ithma 'alayhi innallāha ghafūrur rahīm
Na mwenye kumkhofia muusiaji kwenda kombo au kupata dhambi akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu. 182
Maelezo ya chini
182 Ama ikiwa wasiya umeacha haki na njia iliyo sawa tuliyo kwisha ibainisha, kwa mwenye kufanya wasiya kumharimisha fakiri akampa tajiri, akawawacha jamaa zake akawapa mafakiri wasio rithi watu mbali, basi mwenye kwenda mwendo wa kheri akamrejeza mwenye kufanya wasiya ende sawa, basi hapana dhambi kwa kuugeuza wasiya kwa namna hiyo. Na Mwenyezi Mungu hamchukulii kitu kwa hayo, kwani Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu.