Surat Al-A'raf, aya 77

7:77

فَعَقَرُواْ ٱلنَّاقَةَ وَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ وَقَالُواْ يَٰصَٰلِحُ ٱئۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ ٧٧

Fa'aqarun-nāqata wa'ataw 'an amri rabbihim waqālū yāsālihu'tinā bimā ta'idunā in kunta minal-mursalīn

Na wakamuuwa yule ngamia, na wakaasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayo tuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume. 77

Maelezo ya chini

77 Inda ya wenye kiburi ikakakamia, na wakampinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakamchinja Ngamia. Walivuka mpaka katika kiburi chao, wakaitupilia mbali amri ya Mola wao Mlezi, na wakasema kwa upinzani: Ewe Swaleh! Tuletee hiyo adhabu uliyo tuahidi ikiwa kweli wewe ni miongoni ya alio watuma Mwenyezi Mungu.