Surat Al-A'raf, aya 195

7:195

أَلَهُمۡ أَرۡجُلٞ يَمۡشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَيۡدٖ يَبۡطِشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَعۡيُنٞ يُبۡصِرُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ ءَاذَانٞ يَسۡمَعُونَ بِهَاۗ قُلِ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ ١٩٥

Alahum arjulun yamshūna bihā am lahum aydin yabtishūna bihā am lahum a'yunun yubsirūna bihā am lahum ādhānun yasma'ūna bihā qulid'ū shurakā'akum thumma kīdūni falā tunzirūn

Je, wao wanayo miguu ya kwendea? Au wanayo mikono ya kutetea? Au wanayo macho ya kuonea? Au wanayo masikio ya kusikizia? Sema: Iiteni hio miungu yenu ya ushirikina. Kisha nifanyieni mimi vitimbi, wala msinipe muhula. 195

Maelezo ya chini

195 Bali haya masanamu ni duni kuliko nyinyi kwa kuumbwa na kuwa! Kwani wao wana miguu ya kuendea? Au wana mikono ya kukinga madhara yasikupateni au yasiwapate wenyewe? Au wana macho ya kuonea? Au masikio ya kusikia hayo mnayo yataka wakakupeni? Hawana chochote katika hayo! Vipi basi mnawashirikisha hao na Mwenyezi Mungu? Na ikiwa nyinyi mnadhani kuwa hio miungu ya uwongo inaweza kunidhuru mimi au mtu yeyote, basi iiteni, na mfanye njama zenu pamoja nao kama mtakavyo, bila ya kunipa muhula wala kungoja. Hao hakika hawawezi kitu! Basi msiningojee, na wala mimi siwabali.