يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ قُل لِّمَن فِيٓ أَيۡدِيكُم مِّنَ ٱلۡأَسۡرَىٰٓ إِن يَعۡلَمِ ٱللَّهُ فِي قُلُوبِكُمۡ خَيۡرٗا يُؤۡتِكُمۡ خَيۡرٗا مِّمَّآ أُخِذَ مِنكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ٧٠
Yā'ayyuhan-nabiyyu qul liman fī aydīkum minal-asrā in ya'lamillāhu fī qulūbikum khayran yu'tikum khayram mimmā ukhidha minkum wayaghfir lakum wallāhu ghafūrur rahīm
Ewe Nabii! Waambie mateka waliomo mikononi mwenu: Kama Mwenyezi akiona kheri yoyote nyoyoni mwenu atakupeni bora kuliko vilivyo chukuliwa kwenu, na atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. 70
Maelezo ya chini
70 Ewe Nabii! Waambie hao mateka walio angukia mikononi mwenu: Ikiwa katika nyoyo zenu ipo kheri anayo ijua Mwenyezi Mungu, Yeye atakulipeni yaliyo bora zaidi kuliko hicho walicho kichukua Waumini, na atakusameheni ushirikina wenu na madhambi mliyo kuwa nayo. Na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghfira na rehema kwa mwenye kutubia madhambi yake.