فَكُلُواْ مِمَّا غَنِمۡتُمۡ حَلَٰلٗا طَيِّبٗاۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ٦٩
Fakulū mimmā ghanimtum halālan tayyiban wattaqullāha innallāha ghafūrur rahīm
Basi kuleni katika mlivyo teka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. 69
Maelezo ya chini
69 Basi sasa tumieni mlicho kipata katika fidia kwa kuwa ni halali kwenu, wala si uchumi muovu. Na mcheni Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote. Hakika Mwenyezi Mungu ni mkubwa wa kusamehe na kumrehemu amtakaye katika waja wake pindi akirejea.